Mwanafunzi
wa Tanzania aliyekuwa akisoma nchini Afrika Kusini,Baraka Nafari aliyekuwa
akichukua Shahada ya Uzamivu (PHD) katika Chuo Kikuu cha Johannesburg (UJ)
ameuawa kikatili Ijumaa Februari 23, mwaka huu kwa kugongwa na gari mara mbili
na kubamizwa kwenye ukuta na baadaye kushambuliwa kwa visu.
Kwa
mujibu wa habari hizo za mtandao, kamera za usalama za CCTV za chuo hicho
zilionyesha Baraka na mwanafunzi mwenzake wakikimbia kujiokoa wakati watu
wawili waliokuwa kwenye teksi walipokuwa wakiwakimbiza.
Aidha,
Kamera hiyo iliendelea kumuonyesha dereva teksi huyo akimgonga kwa makusudi
mwanafunzi huyo kwenye uzio wa makazi ya chuo hicho yaliyoko Auckland Park na
kumuua.
Taarifa
hizo zimeongeza kuwa dereva wa gari hilo alikamatwa na polisi kwa kuendesha bila
leseni, lakini baadaye aliachiwa huru bila kufunguliwa mashtaka yoyote.
Hata
hivyo, Msemaji wa Wizara ya Mambo na Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Mindi Kasiga amesema kuwa wizara inafanya mawasilianao na ubalozi wa Tanzania
nchini Afrika Kusini ili kubaini undani wa suala hilo.
0 comments:
Post a Comment