Tuesday 6 March 2018

WAANDAMANA KUOMBA RAIS ADHIBITI ULEVI WA WANAUME….

Mamia ya wanawake katika vijiji vya Kirangi na Kuri Kiambu nchini Kenya, wameandamana Jumapili iliyopita wakipinga ongezeko la vilabu vya pombe (bars) na ulevi wa waume zao.


Wakizungumza wakati wa maandamano hayo ya amani, wanawake zaidi ya 100 wa eneo hilo, walionesha hasira zao dhidi ya ulevi wa wanaume na watoto wao wa kiume.

Ombi la wanawake hao kwa Rais Uhuru Kenyatta, ni kuwachukulia hatua maafisa wa jeshi la polisi katika eneo hilo, ambao wanadaiwa kupokea rushwa ili kulinda kumbi za starehe na bar katika eneo hilo tofauti na jitihada za Serikali kudhibiti ulevi hasa wa pombe haramu.

Walidai wanaume wao wamekuwa dhaifu wanaoshindwa kutimiza wajibu wao wa kifamilia, wengi wao wamekimbia nyumba zao.

Waliongeza kuwa wengine walifikia hatua ya kuuza mali zao ili wapate pesa ya kununua pombe.


Maandamano hayo yamekuja wakati ambapo Serikali ya Kenya imeanza oparesheni ya kuharibu vifaa vya kutengeneza pombe haramu na kuwakamata wahusika.

0 comments:

Post a Comment