Kama ulikuwa hufahamu ni kwamba Korea Kaskazini sasa
hivi hali ya hewa ni joto sana, lakini yapo mengine toka huko ambapo msimu huu
wa joto kali umepewa jina la Sambok.
Limetolewa
agizo na serikali kuwa, Ofisi zote, shule na kila taasisi nchi nzima, zinatakiwa
kufuata ratiba mpya ambayo Serikali imeweka.
Ratiba
hiyo mpya ya sasa ni kwamba kila kitu kitaanza kufanya kazi saa 11 asubuhi
badala ya saa mbili asubuhi, na mwisho wa shughuli zote ni saa saba mchana,
hilo ni agizo jipya la Serikali ya Korea
Kaskazini.
Wastani wa joto la Korea ni
kama 29˚ Centrigrade lakini kwa sasa imefikia mpaka 40˚ Centigrade.
Hii
sio mara ya kwanza kutangazwa utaratibu huo, kwani wakati Rais Kim Jong-il akiwa
madarakani uliwahi kutangazwa utaratibu wa aina hii pia.
Htari nyingine ni kwamba Maofisini kwenye AC na feni,
huenda hii isiwe taarifa nzuri kwao, huku joto likiwa limekuwa kali na hakuna
maji ya kutosha kwenye vyanzo vya umeme sasahivi, kwa hiyo ishu ya feni na AC
kufanya kazi ofisini huenda ikawa kitendawili.
Watu wengi hawajapenda hiyo ratiba mpya, unaambiwa
mpaka Migahawa ya Serikali inatoa huduma mwisho mchana, ukienda jioni au usiku
hakuna huduma utakayopata!!
0 comments:
Post a Comment