Wana
sayansi wa NASA kutoka Marekani wanasema kuwa,majaribio yao ya kurusha chombo
kwenda katika sayari ya Pluto yamekuwa na mafanikio makubwa.
Chombo hicho kimefanikiwa kutuma
taarifa katika kituo cha utafiti huo cha Maryland, zilizochukua takribani saa
nne na nusu hadi kufika duniani na kupokelewa na antenna NASA.
Saa chache zijazo wanasayansi
hawa wa NASA wameeleza kuwa, wanatarajia kupata mfululizo wa taariza zaidi na
picha kutoka sayari hiyo ya Pluto ambazo zitatoa uhalisia wa undani wa sayari
hiyo ya Pluto.
0 comments:
Post a Comment