Nchi chache Afrika zimekubali mapenzi ya jinsia moja |
Msumbiji
imehalalisha mapenzi ya jinsia moja,na kuwa moja wapo wa nchi chache Afrika
zinazohalalisha mapenzi ya jinsia moja.
Sheria hiyo iliyowekwa na wakoloni
wa nchi hiyo Ureno,iliondolewa na bunge la nchi hiyo.
Watetezi wa haki za wapenzi wa
jinsia moja,wametaja hatua hiyo kama ushindi mkubwa.
Hata hivyo nchi nyingi za Afrika
zimeweka sheria kali dhidi ya mapenzi ya jinsia moja.
Nigeria ilipiga marufuku na kuweka
adhabu ya kifungo cha miaka 14 jela kwa wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia
moja.
Uganda nayo imeapa kurejesha sheria
kali kuharamisha mapenzi ya jinsia moja,sheria ya awali ilitupiliwa nje na
mahakama ya kikatiba.
Msumbiji sasa inajiunga na mataifa
mengine ikiwa ni pamoja na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Ivory Coast na
Afrika Kusini ambapo siyo hatia kuwa mpenzi wa jinsia moja.
0 comments:
Post a Comment