Mmoja ya wanenguaji nchini Misri Mnenguaji wa kike nchini Misri amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja kwa kosa la kuonekana kwenye video yenye utata mtandaoni. |
Ametiwa hatiani na mahakama moja
nchini humo kwa kosa la kuchochea ufisadi baada ya kuonekana katika video yenye
utata katika mtandao.
Reda al-Fouly alitiwa mbaroni
mwezi Mei mwaka huu, mara baada ya video hiyo ya miondoko ya Pop kuoneshwa
hadharani na baadaye kudhihakiwa kuwa imeenda kinyume na tamaduni za kiarabu.
Muimbaji huyo wa kike alitakiwa
kufafanua mavazi -aliyoyava kwenye wimbo unaoitwa Sib Eddi au let it go of my
hand.
Mkurugenzi wa video hiyo Wael
Seddiki, aliondoka nchini Misri wakati wimbo huo ulipoanza kupondwa kwenye
mitandao ya kijamii.
0 comments:
Post a Comment