Wanasayansi wa taasisi
ya Marekani ya Uchunguzi wa Anga NASA, wamegundua sayari inayofanana kwa karibu
zaidi na dunia kuliko sayari nyingine zote.
Sayari hiyo iliyopewa
jina la Kepler 452-b ina umri wa miaka bilioni 6, na inazunguka nyota
inayofanana na jua linalozungukwa na dunia.
Wanasayansi wa NASA
wanaamini kwamba upo uwezekano wa viumbe hai, kuishi katika sayari hiyo.
Kepler 452-b
imegunduliwa na chombo cha upelelezi wa anga kinachoitwa Kepler.
Chombo hicho
kilirushwa angani mwaka 2009 kwa lengo la kutafuta sayari zenye vigezo
vinavyofanana na dunia.
0 comments:
Post a Comment