gereza la Guantanamo linamilikiwa na Marekani Ikulu ya White house imesema kuwa mipango ya kulifunga gereza la Guantanamo Bay nchini Cuba imefikia awamu za mwisho. |
Rais Barack Obama anasemekana kupatia
kipaombele suala la gereza hilo, tangu aingie madarakani mwaka wa 2009 lakini
limekumbwa na vizuizi kadhaa.
Rais Obama alitoa agizo la kirais
kufungwa kwa kituo hicho mara moja katika siku yake ya kwanza.
Lakini baraza la Congress lilikataa
kuwahamisha wafungwa wa huko kuwaleta nchini Marekani kutokana na hofu za
kiusalama.
Baadhi ya wadadisi wanaamini kuwa Marekani ilifungua
gereza hilo nje ya ardhi ya Marekani ili wanajeshi wake wapate fursa ya kutumia
mbinu zilizopigwa marufuku katika ardhi yao za kuwahoji wafungwa.
Gereza hilo pia limekumbwa kwa
miaka mingi na madai ya ukiukajji wa haki za binadamu, ambapo njia zilizotumika
kuwahoji wafungwa zimekashifiwa kuwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.
Aidha wafungwa wengi wamedai kuteswa, kupigwa na hata
kulazimishwa kukiri baadhi ya mashtaka.
Wafungwa kadhaa maejaribu kujitoa uhai
kutokana na mateso wanayodai kupata huko.
Wengine wamechukua hatua kama kususia
kula kwa wiki kadhaa kama njia ya kulalamika hali duni ya kibinadamu katika
gereza hilo.
Wengi tayari wamerejeshwa nchini mwao,japo kunao baadhi
ambao wanaaminiwa kuwa hatari zaidi na hivyo hawaja achiliwa.
Msemaji mmoja wa ikulu ya white
house ameambia waandishi kuwa, mipango ya kuwasafirisha wafungwa hao kwa njia
salama imefikia awamu za mwisho na itawasilishwa kwa baraza la Congress, lakini
hakutoa maelezo zaidi.
0 comments:
Post a Comment