Wednesday 22 July 2015

Matumaini ya tiba ya ubongo…….!

Maradhi ya Alzheimer huua seli za ubongo
Data zinasubiriwa kwa hamu kuhusu dawa inayotumainiwa kuponya ugonjwa wa udhoofu wa ubongo (Alzheimer) baadae leo.

Watafiti watatangaza matokeo ya uchunguzi kuhusu matumizi ya dawa aina ya solanezumab, ambayo wagonjwa na wanasayansi wanatuami inaweza kuwa tiba ya kwanza ya kupunguza kasi ya kupungua kwa kazi ya ubongo
Dawa iliyopo kwa sasa inasaidi kupunguza dalili,lakini haisitishi kufa kwa seli za ubongo.

Dr Eric Karran kutoka kituo cha utafiti wa maradhi hayo nchini Uingereza , anasema dawa hiyo inaweza kuhakikishwa kuwa na "uwezo mkubwa".
Maradhi ya Alzheimer yanashambulia seli za ubongo
Maelezo ya uchunguzi kuhusu dawa ya solanezumab, yatatolewa katika mkutano mjin Washington.
Dawa hiyo imekua matumaini makubwa ya malengo ya utafiti unaolenga seli za protini, ziitwazo amyloid ambazo humea kwenye ubongo mtu anapokuwa na maradhi ya Alzheimer.
Inadhaniwa kuwa kuundwa kwa lundo la amyloid baina ya neva za seli, kunasababisha kuharibika na baadae kufa kwa seli za ubongo.
Majaribio ya sawa ya maradhi hayo yanayowakumba mamilioni ya watu duniani,yaligonga
mwamba mwaka 2012.
Hata hivyo wakati kampuni ya Marekani ya Eli Lilly ilipoangalia kwa makini data, ilibainika kuwa kuna ishara inaweza kufanya kazi kwa wagonjwa wanaoanza kupata ugonjwa huo.

0 comments:

Post a Comment