Picha
ya kwanza inaonyesha kwa undani sayari ya Pluto ilivyo imeonyeshwa kwa mara ya
kwanza duniani.
Picha hiyo imepigwa na chombo
kisicho na binadamu kilichotumwa kwenye safari hiyo ambacho kilisafiri umbali
wa kilometa bilion saba na tano.
Chombo hicho jana jumanne kilitua
kwenye sayari hiyo.
Katika mkutano na waandishi wa
habari katika chuo Kikuu cha Johns Hopkins kilichopo Maryland Marekani, Mkuu wa
utafiti wa sayari hiyo Alan Stern hakusita kuonyesha furaha yake.
"Jana ilikuwa ni siku nzuri
na ya kipee kwangu, vipi kwenu."
Mkuu huyo wa utafiti Alan Stern
amesema chombo hicho cha anga kimekusanya taarifa nyingi kutoka kwenye sayari
hiyo.
"Sawa chombo chetu cha New
Horizons kimekwenda sasa zaidi ya mile milioni moja.
Zaidi ya kilometa moja na nusu upande wa pili wa Pluto,
hivyo ndivyo tunavyokwenda kwa haraka tumefikia karibu na sayari hiyo hapo jana
asubuhi.
Chombo chetu cha anga kipo katika hali nzuri, kinafanya
mawasiliano na dunia kwa mara nyingine mara kwa mara kwa masaa kuanzia asubuhi
saa 11 na dakika 50.
Tayari tumepata data kutoka kwenye vifaa vya kisayansi
vipatavyo vitano, na tutatoa taarifa kuhusu matokeo tuliyopata, lakini ukweli
ni kwamba tunachunguza kwa undani, kuna mengi." Amesema Alan Stern.
0 comments:
Post a Comment