Takriban
wanajeshi 23 wa Urusi wameuawa karibu na mji wa Omsk ulioko Siberia,baada ya
jengo la kambi ya kijeshi kuporomoka.
Wanajeshi wengine 19 waliokolewa
kutoka kwa vifusi vya jengo hilo.
Mwanajeshi mmoja aliyeokolewa
ameileza runinga ya Urusi kwamba,wanajeshi walikuwa wamelala wakati wa ajali
hiyo.
Picha za televisheni zilionyesha
sehemu ya jengo hilo la ghorofa nne likiwa limeharibika kabisa huku wanajeshi
wakishirikiana kuondosha vifusi.
Inadhaniwa kwamba ukarabati duni
uliofanyika mwaka jana ndio uliosababisha kuporomoka kwa jengo hilo.
0 comments:
Post a Comment