Monday 15 June 2015

Kasisi basha aishtaki kanisa kumbagua…!!!

Kasisi basha aishtaki kanisa kumbagua

Kasisi mmoja ambaye alinyimwa leseni ya kufanya kazi kama mhudumu katika zahanati ya afya kwa misingi ya kuwa katika ndoa ya jinsia moja,amelishtaki kanisa kwa kumbagua.

Kasisi Jeremy Pemberton alikuwa amewasilisha pendekezo la kutaka kuhudumu kama Kasisi katika kanisa lililoko ndani ya hospitali.
Aidha kasisi Pemberton anadai kuwa maombi yake yalipingwa kwa kinywa kipana na kaimu askofu wa Southwell na Nottingham nchini Uingereza.
Rt Revd Richard Inwood alimkashifu kasisi Pemberton kuwa katika ndoa na mwanaume mwenza ambaye ni kinyume na mafundisho ya kanisa la Church of England.
Tume inayosimamia utoaji kazi nchini Uingereza,inatazamia kuanza kuisikiza kesi hiyo leo.
Wadau wa maswala ya ajira wanasema kesi hiyo inatumiwa kama funzo na mtihani kwa tume hiyo ya ajira ya uingereza iwapo itazingatia haki za wafanyikazi ama zile za mwajiri.
Kasisi Pemberton alikuwa mhudumu wa kwanza kanisani kuoa nchini Uingereza.
Pemberton alifunga pingu za maisha mnamo mwezi wa Aprili mwaka wa 2014.

Askofu Inwood, alimnyima kazi kasisi Pemberton, na kisha akaiandikia barua bodi inayosimamia hospitali hiyo ya Sherwood Forest akiwashauri wasimpe kazi kasisi Pemberton.

0 comments:

Post a Comment