Tuesday 9 June 2015

Mguu bandia wenye hisia wazinduliwa......!!!



 
Watafiti katika chuo kikuu nchini Ausralia,wamevumbua mguu wa kwanza bandia duniani wenye uwezo wa kusisimua hisia halisi za binadamu.

Mguu huo wenye tofauti chache mno na ule halisi unahisi hata maumivu.
Katika uvumbuzi huo wa Profesa Hubert Egger wa chuo kikuu cha Upper Austria,amesema mguu huo bandia unatumia neva za mwili wa mtu aliyekatwa mguu wake.
Bwana Wolfgang Rangger amekuwa na mguu huo bandia kwa miezi sita
 Aidha neva za ncha za mguu wa mgonjwa hushikanishwa na waya zinazowasiliana na ubongo kupitia kwa paja.
Professor Egger anaelezea kuwa bwana mmoja mlemavu amekuwa akiuvaa mguu huo bandia kwa miezi sita sasa.
Bwana Wolfgang Rangger amesema kuwa katika muda huo wa miezi sita,anauwezo wa kubaini iwapo anakanyaga mawe, simiti,na hata nyasi.

0 comments:

Post a Comment