Serikali ya China,imepiga marufuku kuvuta
sigara katika maeneo yote ya wazi katika mji wa Beijing.
Maelfu ya maafisa
wameanza kufanya ukaguzi katika maeneo yote ya wazi na watakaokiuka kufuata
sheria hiyo watapigwa faini.
Hata hivyo China ina wavuta sigara milioni mia tatu wakati sheria ya
kusitisha wavutaji sigara katika maeneo ya wazi ya mji wa Beijing ilipopitishwa
kwa mara ya kwanza na kushindwa kutekelezeka.
Ripoti inasema kuwa watu wengi
wanadhani sheria hiyo ya kukataza kabisa uvutaji sigara haitafanya kazi.
0 comments:
Post a Comment