Wednesday, 10 June 2015

Mtoto azaliwa kutokana na mayai yaliyohifadhiwa kwenye Jokofuu!!!


Mayai ya mwanamke yanapokutana na mbegu ya kiume

Mwanamke mmoja nchini Ubelgiji amekuwa wa kwanza duniani,kujifungua mtoto kwa kutumia upandikizaji wa mayai ya mwanamke yaliowekwa katika jokovu alipokuwa mtoto.

Msichana huyo wa miaka 27 alikuwa na mayai yaliotolewa akiwa na umri wa miaka 13, kabla ya kuanza kupewa matibabu ya anemia ya seli.
Mayai yake yaliosalia yalifeli kutokana na matibabu hayo,hatua ambayo ingeathiri uwezo wake wa kushika mimba bila upandikizaji huo.
Wataalam wanatumai kwamba mpango huo huenda ukawasaidia wagonjwa wengine wadogo.
Mwanamke huyo alijifungua mvulana mwenye afya nzuri mwezi Novemba mwaka 2014, na maelezo kuhusu swala hilo yalichapishwa siku ya jumatano katika jarida la kizazi cha binaadamu.
Mwanamke huyo ambaye hakutaka kujulikana alipatikana na ugonjwa wa anemia ya seli alipokuwa na umri wa miaka mitano.
Alihamia kutoka jamhuri ya Congo na kuelekea Ubelgiji,ambapo madaktari waliamua ugonjwa wake ulikuwa hatari kwa yeye kufanyiwa upandikizaji wa ubongo kwa kutumia tishu za kakaake zinazofanana na zake.

Mwanasayansi wa utafiti
Lakini kabla ya kuanza upandikizaji huo walitakiwa kutumia kemikali ili kutibu mgonjwa huyo kwa lengo la kudhoofisha kinga yake ili kuzuia kutokataa tishu hiyo.
Matibabu ya kutumia kemikali yanaweza kuharibu kazi ya mayai hayo,kwa hivyo walitoa mayai yake ya upande wa kulia na kuyaweka katika jokovu.
Wakati huo,alikuwa akionyesha ishara za kupevuka,lakini alikuwa hajaanza kupata siku zake (hedhi).
Mayai yake yaliosali yalifeli akiwa na umri wa miaka 15.
Miaka kumi baadaye aliamua kwamba angetaka kupata mtoto,hivyo basi madaktari wakapandikiza mayai yake katika mayai yaliokuwa yamesalia na mayai mengine 11 katika sehemu zake nyingine mwilini.
Mgonjwa huo alianza kupata hedhi baada ya miezi mitano na kushika mimba akiwa na umri wa miaka 27.
Mkunga aliyeongoza tiba hiyo ya kumwezesha mgonjwa huyo kuweza kushika mimba Daktari Isabelle Demeestere,alisema kuwa kuna matumaini kwamba mpango huo unaweza kuwasaidia vijana wengine ambao wanakabiliwa na hatari ya kufeli kwa mayai yao ya uzazi,hasa kutokana na ongezeko la idadi ya waathiriwa wa muda mrefu wa magonjwa ya damu wakiwa watoto.

0 comments:

Post a Comment