Monday, 15 June 2015

Wapenzi wakongwe zaidi duniani waoana…!!!

Mwanaume mmoja Muingereza mwenye umri wa miaka 103 ameingia katika daftari za historia kwa kuwa bwana harusi mkongwe zaidi duniani.

Bwana George Kirby alimpiga pambaja bi harusi Doreen Luckie, mwenye umri wa miaka 92 na kula kiapo cha kuwa muaminifu kwake hadi kifo kitakapo watenganisha!
Bwana Kirby alisema kuwa bi Luckie humfanya akajisikia barubaru.
Aidha aliwavunja mbavu waliohudhuria sherehe hiyo aliposema kuwa wakati mwengine umri humlemea.
Kirby na sabuni yake ya roho wamekuwa pamoja kwa takriban miaka 27 sasa,kabla hawajaamua kufunga pingu za maiasha akisema kuwa ''anaona umri unasonga''.
Bi harusi alivalia gauni leupe lenye maua ya samawati,huku Kirby ambaye alikuwa ni bondia shupavu katika ujana wake akivalia suti japo aliletwa madhabahuni akiwa kwenye kiti chenye magurudumu.
Kwa pamoja wawili hao wamevunja rekodi ya dunia ya kuwa maharusi wakongwe zaidi.
Kwa jumla wanaumri wa miaka 195 ambayo ni miaka 7 zaidi ya rekodi ya awali ya maharusi wakongwe.
Rekodi ya awali ilikuwa ikishikiliwa na wapenzi wawili raia wa Ufaransa, Francois Fernandez na Madeleine Francineau.


Related Posts:

  • UJERUMANI YAKABIDHI NDEGE KUKABILI UJANGILI… Serikali ya Ujerumani imetoa msaada wa ndege maalumu aina ya “Husky A-1C Aircraft” kwa Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Malisili na Utalii kusaidia katika doria za kupambana na ujangili katika Pori la Akiba la Selou… Read More
  • WAWILI WAFA KWA KUANGUKIWA NA KIFUSI MACHIMBONI…. Watu wawili wameaga dunia baada ya kuangukiwa na kifusi kwenye machimbo haramu ya dhahabu hapo juzi huko katika mkoa wa Geita. Kamanda wa polisi wa mkoa huo Mponjoli Mwabulambo amethibitisha kuwa ajali hiyo ilitokea maj… Read More
  • APP YA SIMU YA TALIBAN YATOLEWA SOKONI..... Alemarah programu inayotumiwa katika simu za Android iliyoundwa na kundi la wapiganaji wa Taliban, imeondolewa kwenye soko la programu la Google Play Store. App hiyo iliyozinduliwa tarehe 1 Aprili, miongoni mwa mengine i… Read More
  • RIPOTI: DUNIA YAELEMEWA NA WATU WANENE..! Utafiti mpya umeonesha watu wazima wengi duniani ni wanene kupita kiasi na kwamba hakuna matumaini ya kufikia lengo la kupunguza idadi ya watu wanene duniani. Wanasayansi waliofanya utafiti huo ambao walitoka Chuo … Read More
  • ASH SHABAAB YAMNYONGA MTANZANIA…! Raia wa Tanzania Jemes Mwesiga (27) aliyejiunga na kundi la al Shabaab la nchini Somalia, amenyongwa na kundi hilo kwa tuhuma za ujasusi. Mtandao wa habari wa Hiiraan Online umeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, h… Read More

0 comments:

Post a Comment