Friday, 5 June 2015

Ghana yatangaza siku tatu za maombolezo...!!!!!

Kituo cha mafuta kikiwa kimeteketea mjini Accra, Ghana
Ghana imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kufuatia vifo vya watu mia na hamsini vilivyotokana na mafuriko na mlipuko kwenye kituo kimoja cha mafuta.
Mlipuko huo ulitokea hapo jana wakati mamia ya watu walipokuwa wamejihifadhi katika kituo hicho cha mafuta kutokana na mvua kubwa zinazonyesha.
Rais wa Ghana,John Mahama amesema janga halitajirudia tena.
Moto ukiwaka kutokana na mlipuko uliotokea kituo cha mafuta na gesi mjini Accra, Ghana
Bwana Mahama amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mji mkuu ,Accra alipotembelea eneo la tukio.
Amesema watu wanapaswa kuachana na tabia ya kujenga kwenye mikondo ya maji na inabidi utekelezaji ufanyike ili kuzuia janga lingine kama hilo kutokea.
"Tutachukua hatua fulani kuzuia hili lisitokee katika wakati ujao na mara kwa mara. Hatua hizi zinapokuwa kali, mnakuwa na huruma na kutaka zisitekelezwe.
Lakini nafikiri wakati umefika, mnafahamu, kwa kuziondoa nyumba katika maeneo ya maji na umma lazima uelewe kuwa ni lazima kila mtu kuhudumiwa.
Nina maana kupotea kwa maisha kwa namna hii ni janga kubwa ambalo halijawahi kutokea hapo kabla."Anasema Rais Mahama.
Miili ya watu imeendelea kutolewa kutoka eneo la tukio na kuwekwa katika malori. Serikali ya Ghana bado inajaribu kupata idadi kamili ya watu waliokufa au kuathirika kutokana na ajali hiyo.
Wengi wa waliokufa walijihifadhi katika kituo cha petroli kukwepa mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha ambayo imesababisha mafuriko katika sehemu kubwa ya mji wa Accra.

0 comments:

Post a Comment