Rais wa Korea Kusini Park Geun-Hye |
Zaidi ya shule 700 Korea Kusini zimefungwa kuhofia
kuenea kwa ugonjwa uliozuka, unaoshambulia mfumo wa upumuaji uliozuka kutoka
Mashariki ya kati wa MERS.
Watu watatu hadi sasa wanadaiwa kufa kutokana na ugonjwa huo,ambapo pia watu wengine 35 wamebainika kuwa na maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo.
MERS ni mara ya kwanza kugunduliwa nje ya Saudi Arabia, kwani miaka mitatu iliyopita mgonjwa wa kwanza aligunduliwa huko Mashariki ya Kati.
Rais wa Korea Kusini Park Geun-Hye, amehimiza jitihada zaidi kukabiliana na ueneaji wa virusi vya ugonjwa huo.
Raia wa Korea kwa sasa wamekumbwa na wasiwasi kutokana na ugonjwa huo wa SARS ulioua mamia ya watu huko Kaskazini Mashariki mwa Asia,zaidi ya muongo mmoja uliopita.
0 comments:
Post a Comment