Monday 8 June 2015

UN:Eritrea imekiuka haki za binadamu............!!!!


 Umoja wa Mataifa unasema kuwa serikali ya Eritrea inaendesha ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya watu wa nchi hiyo.

Baada ya uchunguzi uliochukua muda wa mwaka mmoja, tume ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa ilisema kuwa mbinu za uongozi zinazotumiwa nchini Eritrea huwaweka watu katika hali ya wasiwasi kila wakati.
Imesema kuwa hali hiyo imesababisha maelfu ya watu kuihama nchi hiyo.
Eritrea inachukua nafasi ya pili baada ya Syria kuwa nchi wanakotoka wahamiaji wengi wanaojaribu kuvuka bahari ya Maditerranean.
Ripoti hiyo inasema kuwa dhuluma zikiwemo mauaji ya kiholela, kukamwata kwa watu, mateso na kazi za lazima ni baadhi ya yale yanayoendelea nchini Eritrea.

0 comments:

Post a Comment