Ikiwa jana waislamu katika maeneo mengi dunia wameanza mwezi mtufu wa ramadhani,nchini chad imetolewa amri ya mtu yoyote kutovaa vazi la hijabu.
Amri hiyo
inatokan na Shambulio la Kigaidi limetokea Chad Jumatatu June 15 2015 katika
Jiji la N’Djamena, huku watu 23 wakiuawana na wengine zaidiya 100 wakipata
majeraha makubwa.
Waziri Mkuu wa Chad Kalzeube Pahimi Deubet,amesema
mtu aliyelipua mabomu hayo alitumia vazi ambalo linavaliwa na wanawake wa
kiislamu ambalo linaziba mpaka usoni.
Agizo hilo limetolewa jana June 18 2015 hivyo hakuna
mtu yoyote anaeruhusiwa kuvaa vazi hilo popote ndani ya Chad.
Japo haijathibitika ni nani kahusika na Shambulio
hilo, stori mpaka sasa kutoka Chad zinataja sana kundi la Boko Haram kutokana na kitendo cha nchi hiyo
kuisaidia Nigeria kupambana na Kundi hilo la wapiganaji.
0 comments:
Post a Comment