Rais Jacob Zuma |
Tarehe 19 June mwaka huu Bunge la South Africa liliingia kwenye headlines katika
vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii baada ya baadhi ya viongozi
kutoka chama cha upinzani kuanzisha vurugu zilizo pelekea kuairishwa kwa Bunge
hilo siku ya ijumaa.
Bunge tukufu la South
Africa liliingia
vurungu baada ya wanachama wa Economic
Freedom Fighters kumzuia
rais Jacob
Zuma kuendelea
kutoa ripoti aliokusudia kuwasilisha mbele ya bunge hilo kwa kumshambilia
rais huyo na maswali yanayohsu uwajibikaji wake, maswali ambayo
yaliongaishwa na malalamiko ya yeye kukiuka katiba ya nchi hiyo, kitendo
kilichopelekea rais huyo kutokupewa nafasi ya kujieleza.
Kitendo hichi kilimlazimu spika wa bunge Baleka Mbete kuairisha Bunge hilo na kuita kikao cha dharula na
vyama hivyo nje ya bunge hilo baada ya vurungu kutapakaa bungeni hapo, na
alipohojiwa na vyombo vya habari, Spika wa bunge la South Africa alisema amesikitishwa na kitendo hiki kufanyika na baadhi ya
watu wanaotazamwa na jamii kama viongozi, na kuongezea kua, kitendo hichi
sio mara ya kwanza kutokea kwani kitu kama hiki kilishawahi kutokea mwezi Agosti tarehe 21 mwaka jana ambako pia alilazimika
kuairisha bunge hilo kutokana na vurungu kuanzishwa na vyama vya upinzani.
Bunge la South Africa limepinga baadhi ya malalamiko kutoka
kwa viongozi wa vyama vya upinzani kua rais Jacob
Zuma anakiuka
katiba na kuepuka uwajibikaji na kusema kua rais huyo anategema kuonekana tena
bungeni mwezi Agosti mwaka huu kwa ajili ya kutoa ripoti
hio kama sheria ya nchi inavyomtaka kufanya hivyo mara nne kwa mwaka na mara
moja kwa mwaka katika Baraza la taifa la majimbo.
0 comments:
Post a Comment