Madereva wa kiume wa pikipiki maarufu kama bodaboda na wengine
wanaotumia usafiri huo kwa muda mrefu wapo katika hatari ya kuwa wagumba.
Tafiti
nyingine zilizofanywa zinazonyesha kuwa huenda wakakabiliwa na uhaba wa mbegu
za kiume na hatimaye kushindwa kutoa mbegu za kiume zenye uwezo wa kutunga
mimba.
Hali
hiyo inatokana na sehemu za siri zinazozalisha mbegu,muda mwingi kuwa katika
hali ya joto kitu ambacho kitaalamu kimebainisha kuwa kinafanya mishipa ya damu
kutofanya vyema na kuchochea uzalishaji mbegu hizo.
Maelfu
ya vijana nchini wamejiajiri kupitia usafiri wa bodaboda, huku wengi wakiwa
katika umri mdogo wa kati ya miaka 18 hadi 50, kutokana na tafiti hizo huenda
Tanzania ikaathirika zaidi kwa kuwa na vijana wengi wanaoweza kuwa wagumba.
Utafiti
unaonyesha kuwa vijana wengi wanaokaa katika kiti cha pikipiki hupambana na
joto,kutokana na ngozi laini iliyopo katika korodani,mirija ya damu hushindwa
kupitisha virutubisho kutokana na msuguano mkali uliopo.
0 comments:
Post a Comment