Friday 26 June 2015

Alioa siku 3 tu kabla ya kuaga dunia……!!

Alioa siku 3 tu kabla ya kuaga dunia
Kijana mmoja barubaru alimuoa mpenzi wake siku tatu tu kabla yake kuaga dunia kutokana na Saratani ya damu lukaemia.

Omar Al Shaikh alimuoa mpenzi wake Amie Cresswell wote wenye umri wa miaka 16, katika wadi ya hospitali kuu ya Malkia Elizabeth ilioko Birmingham Uingereza.
Omar aliaga dunia Jumatatu hii siku tatu tu baada ya kufunga pingu za maisha na Amie.
Omar aliaga dunia baada ya kukosa mtu ambaye damu yake inayoingiana na yake.
Omar alimchumbia Amie baada ya kufahamishwa na madaktari kuwa alikuwa na siku 5 tu za kuishi.
Mamake bi Mirabela anasema kuwa mwanae alijizatiti hadi siku yake ya mwisho,na yeye alijikaza sana na kupanga kila kitu alichotaka kifanyike.
Mama yake anasema mwanae alitaka sana kumuoa Amie,alikuwa akinieleza kuwa angefurahia sana akisimama mbele ya haki na kumweleza mwenyezi mungu kuwa Amie alikuwa ni mkewe'
Shangazi yake Anca Dumitriu amesema "Ilikuwa ni siku nzuri sana kwani wote walifurahia sana pale Omar alimwambia Amie ''Wewe ni mke wangu sasa.'
Kijana huyo aligunduliwa kuwa anaugua Lukemia baada ya kuanguka na kuzirai alipokuwa akicheza mpira.
Kutokana na asili yake ya Kirumi na Kiarabu,ilikuwa vigumu sana kupata mtu mwenye chembechembe zitakazoingiana.

Mamake amesema tangu afahamishwe kuhusu kuzoroteka kwa hali yake ya siha mapema mwezi huu, Omar amejitahidi kuwa mchangamfu hadi alipoaga dunia.

0 comments:

Post a Comment