Tuesday 9 June 2015

Bahari ni kubwa lakini ustahimili wake wa uchafuzi ni mdogo…



 
Licha ya kwamba eneo la bahari duniani ni kubwa,bado uwezo wake wa kustahimili uchafuzi utokanao na shughuli za binadamu ni mdogo.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika ujumbe wake wa siku ya bahari duniani ambayo ilikuwa jana.
Amesema bahari ni muhimu katika mustakhabali wa sayari ya dunia,hivyo matumizi endelevu ya rasilimali zake na kuepuka uchafuzi hasa unaotokana na shughuli za binadamu, ni lazima vipatiwe ufumbuzi kwa ustawi wa kizazi cha sasa na vijavyo.
Umoja wa Mataifa unataja mabadiliko ya tabianchi kuwa kitisho kikubwa zaidi kwa ustawi wa bahari, lakini David Osborn Mkurugenzi wa maabara za mazingira kwenye shirika la kimataifa la nishati ya atomiki IAEA, anasema kile ambacho binadamu anaweza kufanya ili kubadili mwelekeo.
 
Amesema Wananchi wanaweza kutimiza wajibu wao kwa kuchukua hatua za kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi.
Halikadhalika, wanaweza kuchukua hatua kupunguza uchafuzi. Fikiria wanavyotupa taka zao, mathalani plastiki. Kwa hiyo hii ni mifano ya mambo tunaweza kufanya.
Tunaweza kuamua kula samaki waliovuliwa kiendelevu. Kwa hiyo tujielimishe ni aina gani wavuliwa kwa njia hiyo."
Bwana Osborne amefafanua kuwa licha ya kwamba kuna bahari zinazotambuliwa kwa majina mbali mbali mathalani, Pasifiki na Hindi lakini bahari ni moja tu duniani na hivyo itambuliwe kwa umoja.

0 comments:

Post a Comment