Watoto
wawili wenye umri wa kati ya miaka miwili na mitano wameuawa na fisi katika
Kijiji cha Mnkola, Kata ya Ibihwa wilayani Bahi Mkoa wa Dodoma katika matukio
mawili tofauti.
Mwenyekiti
wa Kitongoji cha Teya Kata ya Ilindi wilayani hapa, Paul Mwaja alisema kuwa
watoto hao wameuawa katika matukio mawili ndani ya kipindi cha wiki moja.
Mwaja
alisema tukio la kwanza lilitokea juzi ambapo mtoto mmoja wa kiume mwenye
aliuawa na fisi wakati akiwa na wenzie wawili wamelala.
Alisema
usiku wa kuamkia jana, fisi huyo alirudi tena katika kijiji hicho na
kumnyang’anya mama mmoja mtoto wake mdogo mwenye umri wa miaka miwili.
Mwaja
alisema fisi huyo alimla mtoto huyo na kumbakisha kichwa na utumbo tu, hali
iliyozua taharuki katika kijiji hicho.
Hata
hivyo, alisema baada ya tukio hilo wananchi waliamua kufanya msako na kumkamata
fisi huyo na kumuua.
Baba mzazi
wa mtoto aliyeuawa usiku wa kuamkia jana aliyejitambulisha kwa jina moja la
Mchamingi, alisema hawana imani kama fisi huyo kama ni wa kawaida kwani katika
tukio la kwanza kabla ya kuuawa, alikimbilia katika kijiji jirani cha Bahi
Makulu na kupotelea kwenye nyumba za watu.
0 comments:
Post a Comment