Wednesday 10 June 2015

Watawa wakwama ndani ya lifti kwa siku 3…



 
Watawa wawili wameokolewa kutoka kwa lifti mjini Rome,baada ya kukwama kwa siku tatu bila chakula wala maji.

Wawili hao mmoja wa miaka 69 raia wa New Zealand na mwingine wa umri wa miaka 58 raia wa Ireland, walikwama ndani ya lifti hiyo siku ya Ijumaa baada ya kutokea kwa hitilafu ya umeme.
Watawa hao waligunduliwa siku ya Jumatatu wakati mfanyikazi mmoja kuwaita polisi,alipokosa kujibiwa baada ya kufinya kengele ya mlango.

0 comments:

Post a Comment