Wakazi
wa kitongoji duni cha Mathare katika mji mkuu wa Kenya Nairobi, sasa wanaweza
kupata maji safi ya kunywa na kwa matumizi mengine.
Mpango unaoungwa mkono na
serikali umezinduliwa kwenye mji mkuu wa Kenya Nairobi, unaowawezesha watu
wanaoishi kwenye mitaa ya mabanda kununua maji kwa kutumia kadi.
Vituo vya kuuza maji vimebuniwa
kote katika sehemu za mabanda,ambapo wenyeji hutumia kadi zilizo na pesa
kununua maji safi na kwa bei nafuu.
Wenyeji wa mitaa ya mabanda nchini Kenya,wamekuwa na
tatizo la kupata maji safi ambapo hulazimika kununua maji kwa bei ghali kutoka
kwa wauzaji au kutoka kwa magenge ambayo hudhibiti na kuuza maji hayo kwa
kuyachuuza.
Mradi kama huo umefaulu katika
baadhi ya maeneo ya vijijini nchini Kenya, lakini hii ni mara ya kwanza
kuzinduliwa katika mji huo mkuu.
Vituo hivyo vya kutoa huduma hiyo ya maji, vimefanikiwa
kutokana na ushirikiano kati ya serikali ya mitaa nchini Kenya na kampuni ya
maji ya Grundfos ya Denmark.
Kampuni ya kusimamia huduma ya
usambazaji maji,ina mikakati ya kuhakikisha kuwa huduma hii walioianzisha
itasambazwa kote katika mji mkuu wa Nairobi na kwengineko nchini humo.
0 comments:
Post a Comment