Tuesday 23 June 2015

Mazungumzo ya amani Burundi kuanza tena…

Rais Pierre Nkurunziza
Mazungumzo ya kutafuta amani nchini Burundi, yanatarajiwa kuanza tena leo baada ya kusitishwa kwa siku kadhaa.
Mazungumzo hayo ni kati ya serikali, vyama vya upinzani na makundi ya kutetea haki za kibinaadamu, yenye lengo la kumaliza mgogoro wa kisiasa uliozuka kufuatia azma ya Rais Pierre Nkurunziza ya kuwania muhula wa tatu.

Mazungumzo hayo yanasimamiwa na msuluhishi mpya Abdoulaye Bathily kutoka Senegal.
Kutoka Bujumbura Burundi sikiliza taarifa ya Ramadhan Kibuga anasimulia.

0 comments:

Post a Comment