Wednesday 24 June 2015

Kondomu inayotambua maambukizi ya Zinaa...!!

Wanafunzi katika shule moja nchini Uingereza, wameunda mipira ya kondomu inayowaonya watumiaji wanapojamiana na mtu aliyeambukizwa maradhi ya zinaa.

Kondomu hiyo inabadili rangi pindi inapokutana na majimaji ya mtu anayeugua maradhi ya zinaa.
Kondomu hiyo S.T.EYE inaweza kutambua maambukizi ya Chlamydia Kaswende na Kisonono.
Kulingana na wanafunzi hao, kondomu hiyo inabadili rangi tofauti kulingana na bakteria iliyopo.
Uvumbuzi huu ni wa Daanyaal Ali 14, Muaz Nawaz 13 na Chirag Shah 14, ambao ni wanafunzi katika shule ya Isaac Newton Academy iliyoko Ilford, Essex nchini Uingereza.
Wanafunzi hao tayari wametunukiwa, tuzo la ubunifu la ''the TeenTech'' .

Wanafunzi hao walitunukiwa pauni elfu moja pamoja na fursa ya kuzuru Kasri la Malkia wa Uingereza Buckingham Palace.

Muasisi wa kampuni ya ubunifu wa kiteknolojia TeenTech Bwana Maggie Philbin, amesema kuwa,ni wajibu kwa jamii kuchochea ubunifu unaopatikana madarasani kuchochewa na kupigwa msasa kwa minajili ya kuboresha maisha ya mwanadamu.'

0 comments:

Post a Comment