Friday 19 June 2015

Watu 25 wafa kwa kunywa gongo India..!!!

Mtu aliyekunywa pombe haram akihudumiwa
Watu wapatao 25 wamekufa katika mji wa Mumbai nchini India, baada ya kunywa pombe haramu aina ya Gongo na wengine wengi wamelazwa hospitali.

Waziri kiongozi wa jimbo la Maharashtra, ametaka ufanyike uchunguzi na tayari watu watatu wamekamatwa.
Pombe haramu aina ya gongo inayotokana na mahindi inanyweka kwa kiasi kikubwa nchini kote India, ambako wakati mwingine pombe hiyo inauzwa chini ya dola moja ya Kimarekani, ikisababisha vifo vya mara kwa mara.

Karibu watu 170 wameripotiwa kufa katika jimbo la Bengal baada ya kunywa pombe hiyo maarufu kama "moonshine"

0 comments:

Post a Comment