Makao makuu ya Umoja wa Afrika, Addis Ababa,Ethiopia |
Umoja wa
Afrika umesema hautawapeleka waangalizi wake wa uchaguzi katika uchaguzi wa
wabunge wa Burundi, unaofanyika leo kwa sababu masharti ya uchaguzi huru na wa
haki hayajazingatiwa.
Vyama vya upinzani vimesusia uchaguzi wakipinga uamuzi wa
Rais Pierre Nkurunziza wa kugombea muhula wa tatu katika uchaguzi wa rais mwezi
ujao.
Mapema Jumapili Spika wa bunge la Burundi Pie Ntavyohanyuma,
amesema alikimbia nchi yake kwa sababu ya kuhofia usalama wa maisha yake baada
ya kumshauri rais asigombee tena.
Jaribio la Bwana Nkurunziza kupata muhula wa tatu limekumbana
na wimbi la ghasia ambapo zaidi ya watu sabini wameuawa.
0 comments:
Post a Comment