Thursday 25 June 2015

Mtoto auwawa baada ya kubakwa Dar…………


Mtoto anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka mitano hadi sita, ameuwa kikatili jijini Dar es salaam baada ya kubakwa na kisha kunyongwa shingo huku akidaiwa kunyofolewa sehemu za siri.

Mwili wa mototo huyo unadaiwa kutelekezwa katika moja ya nyumba iliyokuwa haijaisha,na kugunduliwa na kijana aliyekuwa akiokota chupa tupu za maji eneo la tabata kisiwani, Dar es salaam.
Baadhi ya mashuhuda wamesema  walilaani tukio hilo na kusema na ukatili  huo ni wa kwanza kutokeo mtaani hapo.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo Christopher Victory, amekiri kutokea kwa tukio hilo na ofisi yake ilipokea taarifa hizo juzi na kulazimika kutoa taarifa kituo cha Polisi cha Tabata.

Kamanda wa Polisi Ilala Lukas Mkondya, amesema taarifa ya unyama huo itawekwa wazi leo baada ya kupokea ripoti ya daktari.

0 comments:

Post a Comment