Tuesday, 19 April 2016

ATOLEWA KWENYE NDEGE KWA KUONGEA KIARABU……

Mwanafunzi wa chuo kikuu raia wa Iraq katika jimbo la California nchini Marekani, anasema kuwa
alitolewa kutoka kwenye ndege ya shirika la ndege la Southwest baada ya kufanya mazungumzo kwa lugha ya kiarabu.
Shirika hilo la Southwest lilisema kuwa mwanafunzi huyo aliondolewa kwenye ndegeni tarehe 9 mwezi Aprili kabla ya ndege hiyo kupaa.
Bw Makhzoomi anasema alikuwa akizungumza na mjomba wake kwa njia ya simu, kuhusu hotuba ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.
Anasema kuwa mwanamke mmoja kwenye ndege hiyo alimkodolea macho wakati alitamka jina Inshallah akimaanisha Mungu akipenda.
Baada ya kutumia jina hili mfanyikazi wa shirika la Southwest alimtoa na kumsindikiza nje ya ndege hiyo..
Bw Makh zoomi ambaye aliingia nchini Marekani kama mkimbizi kutoka Iraq na sasa ni mwanafunzi wa chuo kimoja cha Carlifonia, amesema kuwa hawezi kuingia tena kwenye ndege hiyo.

 

Related Posts:

  • MJI WA MADINA WASHAMBULIWA…!! Mshambuliaji mmoja wa kujitoa mhanga, amejilipua katikati ya Jiji la Media jirani na Msikiti wa Mtume. Jiji la Medina ni miongoni mwa miji mitakatifu, kwa mujibu wa Imani za dini ya Kiislamu. Kituo cha Televisheni… Read More
  • MAJAJI WAJINOA MAHAKAMA YA UFISADI…!! Jaji Mkuu wa tanzania Mohamed Chande amesema kuwa, jopo la majaji linatarajiwa kuingia darasani ili kujifunza sheria mpya ya kuendesha kesi za ufisadi.  Kesi hizo zitakuwa zinaendeshwa katika Mahakama Kuu Kite… Read More
  • MUSEVENI ASIMAMISHA MSAFARA WAKE KUPOKEA SIMU…!! Rais wa Uganda bwana Yoweri Kaguta Museveni, amezua kihoja katika kijiji kimoja karibu na mpaka wa Uganda na Tanzania aliposimamisha msafara wake wa magari iliapokee simu faraghani. Amini usiamini Rais Yoweri Museveni a… Read More
  • OBAMA AMALIZA MUDA WAKE IKULU YA WHITE HOUSE.. Rais Barack Obama wa Marekani amekuwa na mkutano wake wa mwisho na waandishi habari Ikulu mjini washington, tukio la mwisho la shughuli zake rasmi , kabla ya kumkabidhi madaraka Rais mteule Donald Trump. Obama aligusia … Read More
  • MAMIA KUPIGWA PICHA ZA UTUPU UINGEREZA Mamia ya watu watavua nguo zao na kupigwa picha wakiwa tupu kusherehekea utamaduni katika mji wa Hull, Uingereza. Tukio hilo litakuwa la kusherehekea mji huo kama Mji wa Utamaduni. Washiriki watapakwa rangi ya samawati … Read More

0 comments:

Post a Comment