Thursday 7 April 2016

FACEBOOK YATUMIKA KUUZA SILAHA LIBYA…

Utafiti mpya umebaini kwamba kuna soko linaloendelea kuimarika katika biashara haramu ya
bunduki nchini Libya, kupitia mitandao ya kijamii hususan ule wa Facebook.
Ripoti hiyo iliyoangazia miezi 18, ilibaini mauzo ya vifaa vingi kutoka bunduki hadi makombora ya kutungua ndege.
Vifaa hivyo vilikuwa vikiuzwa kupitia mitandao ya siri ya makundi ya Facebook.
Uuzaji wa bunduki ni ukiukaji wa sheria za huduma ya mtandao huo, na msemaji wa Facebook amesema kuwa wanawataka watu kuripoti kuhusu machapisho kama hayo.
Ripoti hiyo ilizinduliwa na utafiti wa silaha ndogo ndogo na data, iliochunguzwa na shirika la utafiti la Armament katika mauzo elfu 1mia 3 na 46.
Watafiti wanaamini kwamba hicho ni kipande kidogo cha biashara yote, inayoendelea katika mitandao ya kijamii.
Kanali Muamar Gaddafi alikuwa mnunuzi mkubwa wa silaha na alidhibiti soko la silaha.
Katika kipindi cha miaka 40 alichokuwa mamlakani,inakadiriwa alitumia dola bilioni 30 kununua silaha.


0 comments:

Post a Comment