Thursday 7 April 2016

VIROBA VYAPIGWA MARUFUKU ARUSHA..!

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Felix Ntibenda, amepiga marufuku uuzwaji wa kilevi aina ya kiroba katika mkoa wake.



Amesema uamuzi huo unatokana na vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa, kushindwa kufanya kazi na kulewa wakati wa kazi.
Aidha mkuu huyo wa mkoa amesema anafanyia kazi sakata la mkazi wa Kata ya Ngarenaro anayedaiwa kujihusisha na uuzaji na uingizaji wa dawa za kulevya, ambaye baada ya kukamatwa na polisi aliachwa katika mazingira ya kutatanisha.
Ntibenda amesema hayo jana Arusha wakati akizungumza na watendaji wa serikali za mitaa, maofisa watendaji kata pamoja na wenyeviti wa serikali za mitaa.
Amesema suala la kilevi aina ya kiroba ni kero kwa vijana kufanya kazi wakiwa wamelewa, au kuwa navyo mifukoni hasa madereva wa pikipiki, daladala na wapiga debe.

Amesema kutokana na vijana kunywa kinywaji hicho nyakati za kazi, amepiga marufuku uuzwaji wa kilevi hicho, atakayekiuka agizo hilo hatua za kisheria zitachukuliwa.

0 comments:

Post a Comment