Wednesday, 27 April 2016

KICHAA CHA MBWA HUU WATU ZAIDI YA 1000 KILA MWAKA NCHINI….

Imeelezwa kuwa watu elfu 1 mia 6 hasa watoto hufa nchini kila mwaka, kutokana na ugonjwa wa
kichaa cha mbwa.

Hayo yalielezwa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Mary Mashingo.
Dk Mashingo amesema vifo hivyo hutokana na wagonjwa hao hasa watoto kukosa chanjo kwa wakati.
Na hiyo ni kutokana na kuwepo kwa vituo saba pekee hapa nchini,ambavyo  vinatoa huduma hizo.


Ameitaja mikoa ambayo vituo hivyo vipo kuwa ni Dar es Salaam, Tabora, Mwanza na Mikoa ya Kusini.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment