Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THDRC), umempa tuzo
ya mwaka George Mgoba aliye mahabusu akikabiliwa na
shtaka la kuandaa kinyume
cha sheria maandamano ya vijana, waliomaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa
(JKT) kushinikiza kupatiwa ajira.
Mgoba amepata tuzo hiyo ya mwaka
kutokana na juhudi alizozifanya
2015 za kuwatetea vijana waliokuwa wanataka kuandamana, kushinikiza Serikali kutoa
ajira kwa vijana waliomaliza mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa THDRC Onesmo Ole
Ngurumwa, amesema suala la haki za binadamu linabaki pale pale bila ya kujali
mhusika amefanya nini, na anastahili adhabu gani iwapo itathibitika ana hatia.
Amesema utatuzi wa tatizo la
ukiukwaji wa sheria kama upo uangaliwe ni kwa kiasi gani unafanyika bila
kuathiri maisha ya binadamu na kumuondolea thamani yake.
Kauli mbiu ya mwaka huu inasema Tuwalinde Watetezi wa Haki za
Binadamu”, ndiyo maana tumeona ni fursa ya kumkumbuka Mgoba ambaye hadi sasa
anaumwa na bado ni mahabusu kwa zaidi ya mwaka, kwa kuwa na alipata matatizo
hayo akiwa anatetea haki za wengine na yake kama binadamu.
0 comments:
Post a Comment