Monday 25 April 2016

JENERALI WA JESHI NA MKEWE WAUAWA BURUNDI..!!

Afisa mkuu wa jeshi la Burundi ameuawa pamoja na mkewe, baada ya kushambuliwa na watu
wasiojulikana mjini Bujumbura.

Jenerali Athanase Kararuza na mkewe wameuawa wakiwapeleka watoto wao shuleni, afisa mmoja wa usalama ambaye hakutaka jina lake litajwe ameambia shirika la habari la AFP.
Wizara ya ulinzi imethibitisha kifo chake.

Jenerali huyo ndiye afisa wa karibuni zaidi wa jeshi kuuawa katika mji huo mkuu wa Burundi tangu kufanyika kwa jaribio la kupindua serikali ya Rais Pierre Nkurunziza mwaka jana

0 comments:

Post a Comment