Monday 4 April 2016

APP YA SIMU YA TALIBAN YATOLEWA SOKONI.....

Alemarah programu inayotumiwa katika simu za Android iliyoundwa na kundi la wapiganaji wa Taliban, imeondolewa kwenye soko la programu la Google Play Store.

App hiyo iliyozinduliwa tarehe 1 Aprili, miongoni mwa mengine ilikuwa na taarifa rasmi na video kutoka kwa kundi hilo la Kiislamu kwa lugha ya Pashto.
Kundi hilo limesema kumetokea “hitilafu za kiufundi” baada ya app hiyo kutoweka.
Hata hivyo imefahamika kwamba app hiyo imeondolewa kwa sababu inakiuka kanuni na sera za Google zinazokataa uchochezi.
App hiyo iligunduliwa na shirika la Marekani la Site Intel Group, linalofuatilia shughuli za makundi ya kijihadi.
Google imekataa kuzungumzia app hiyo binafsi lakini ikasema kupitia taarifa kuwa: “Sera zetu zimeundwa kuridhisha wateja wetu na watu wanaotengeneza app.
Ndio maana huwa twatoa apps zinazokiuka sera hizi kutoka kwenye Google Play.
Msemaji wa kundi la Taliban alikuwa ameambia Bloomberg kwamba, app hiyo ilikuwa sehemu ya juhudi za kiteknolojia za kufikia watu zaidi duniani.

0 comments:

Post a Comment