Mke wa Rais mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki Lucy Kibaki,
amefariki dunia leo jijini London, Uingereza alipokuwa akipatiwa matibabu.
Kwa mujibu wa taarifa ya Rais
Uhuru Kenyatta, Lucy Kibaki amefariki katika hospitali ya Bupa Crowmwell ya
jijini London.
Hali ya mheshimiwa (Lucy) haikuwa
nzuri takribani mwezi mmoja uliopita, na amekuwa akipatiwa matibabu Kenya na
hatimaye Uingereza taarifa iliyosainiwa na Rais Kenyatta imeeleza.
Mke huyo wa Kibaki alilazwa
hospitali ya Nairobi mwezi uliopita, baada ya kuhamishwa akitokea hospitali ya
Gertrude iliyopo Muthaiga.
0 comments:
Post a Comment