Wednesday 13 April 2016

SERIKALI YAZIDI KUSISITIZA KUFUNGA SIMU BANDIA….

Serikali imesisitiza kuwa azma yake ya kuzifunga simu za bandia ifikapo Juni 16 mwaka huu iko
palepale, huku ikiwataka wananchi waache kuzitumia ili kuepuka madhara kwa afya zao.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dk Yahaya Simba, ametoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ukomo wa matumizi ya simu bandia nchini.
Simba amesema agizo la kuzifungia simu hizo lilitolewa tangu Desemba mwaka jana, hivyo kuwapa muda wa miezi sita wananchi kuhakiki simu zao.
Amesisitiza kuwa ifikapo Juni 16 wafanyabiashara watalazimika kuziondoa sokoni simu bandia kwa kuwa zitazimwa.
Mwanasheria wa Tume ya udhibiti na Uzuiaji wa Bidhaa Bandia Tanzania (FCC) Khadija Ngasongwa, amesema wamewasiliana na kampuni zinazotengeneza simu duniani ili kujua tofauti ya bidhaa zao halisi na za bandia.
Amewataka wananchi ambao wamegundua kuwa simu zao siyo halali waache kuzitumia kwa kuwa zina madhara makubwa kwa afya zao, ikiwamo kulipuka na kuwasababisha majeraha au vifo.

0 comments:

Post a Comment