Thursday 21 April 2016

CANADA KUHALALISHA MATUMIZI YA BANGI..!!

Serikali ya Canada itabuni sheria mpya mwaka ujao, ambazo zitahalalisha uuzaji wa bangi.

Iwapo sheria hiyo itaidhinishwa italiorodhesha taifa la Canada, miongoni mwa mataifa yenye uchumi mkubwa magharibi kukubali matumizi wa bangi.
Waziri mkuu Justin Trudeau alipigania dawa hiyo kuhalalishwa, wakati wa kampeni.
Waziri wake wa afya amesema kuwa anataka dawa hiyo kutowafikia watoto pamoja na wahalifu.
Serikali imeahidi kufanya kazi na maafisa wa polisi, ili kuwadhibiti wale wanaouziwa dawa hiyo, wakati inapouzwa na vile inavyotumiwa na wametafuta njia ya kudhibiti dawa hiyo kupitia sheria za uuzaji wa pombe.
Hatahivyo wapinzani wanasema kuwa hatua mbaya zaidi kwa vijana, ni kuruhusu utumiaji wa dawa hiyo ya kulevya.

Utumizi wa bangi nchini humo utasalia kuwa marufuku, huku sheria za kuhalalisha zikiendelea kutengenezwa.

0 comments:

Post a Comment