Wednesday 6 April 2016

IRAN, PAKISTAN NA SAUDIA ZINAONGOZA KWA KUNYONGA…..

Shirika la haki za kibibaadamu la Amnesty International limesema kuwa, kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu walionyongwa ulimwenguni mwaka uliopita, ikilinganishwa na kipindi chochote tangu mwaka 1989.

Takriban watu elfu 1 mia 6 na 34 walinyongwa mwaka 2015,ikiwa ni ongezeko la asilimia 50 ikilinganishwa na mwaka wa 2014.
Imeelezwa kuwa nchi za Iran, Pakistan na Saudia Arabia, walihusika na asilimia 89 ya watu wote walionyongwa duniani.
Jumla hiyo haishirikishi China ambapo Amnesty International imesema kuwa,maelfu zaidi waliuawa lakini rekodi zake zikafichwa.
Kwa upande mwengine kundi hilo limesema kuwa kwa mara ya kwanza, mataifa mengi duniani yalifutilia mbali hukumu ya kunyonga.
Mataifa ya Fiji, Madagascar,Congo Brazaville na Suriname, yalibadilisha sheria zao mwaka 2015, huku Mongolia ikipitisha sheria mpya itakayoanza kutekelezwa baadaye mwaka huu.

Amnesty International imesema kuwa China bado inaongoza miongoni mwa mataifa yanayonyonga watu.

Inakadiriwa kwamba maelfu ya watu walinyongwa,huku maelfu ya wengine wakipewa hukumu ya kunyongwa mwaka 2015.

0 comments:

Post a Comment