Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema kuwa,watanzania
milioni 2.3 kati ya watu milioni 22.3 ambao ndio nguvu kazi ya taifa hawana
ajira.
Kiwango hicho cha ukosefu wa ajira kwa mujibu wa NBS,ni
sawa na asilimia 10.3 ya nguvu kazi ya taifa.
Kiwango hicho kinaelezwa kuwa kimepungua kutoka
asilimia 11.7 ya mwaka 2006.
Hata hivyo utafiti huo
umebainisha kuwa watu ambao hawana ajira, wamebainika wanatumia muda mrefu
zaidi kusaka ajira.
Kwenye utafiti huo imebainishwa kuwa kiwango cha
ukosefu wa ajira kwa muda mrefu, kimeongezeka kutoka asilimia 17.9 mwaka 2006
hadi asilimia 32.5 mwaka 2014.
Utafiti huo pia unaonyesha kuwa wanawake ndio kundi
kubwa la Watanzania ambao wana kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira kuliko
wanaume.
Pia utafiti huo unaonyesha kuwa asilimia 17.2 ya watu
ambao wana uwezo wa kufanya kazi, hawana kazi na wala hawako tayari kufanya
kazi yoyote ya kiuchumi.
Katika kundi hilo wamo wanawake ambao wengi wao
wanajishughulisha na shughuli za nyumbani.
0 comments:
Post a Comment