Thursday 28 April 2016

MTOTO WA MIAKA 2 AMUUA MAMAKE KWA BUNDUKI..!!

Mvulana wa umri wa miaka miwili amempiga risasi na kumuua mamake kimakosa, katika mji wa Milwaukee nchini Marekani.

Mtoto huyo alipata bunduki hiyo sehemu ya nyuma ya gari.
Mwanamke huyo Patrice Price 26 alikuwa akiendesha gari la mpenzi wake ambaye ni mlinzi, ambaye alikuwa ameacha bunduki yake kwenye gari.
Polisi wa Milwaukee wanasema mwanamke huyo alipigwa risasi moja kutoka nyuma,alipokuwa  akiendesha gari mapema Jumanne asubuhi.
Mamake Price na mwanawe mwingine wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja, walikuwa kwenye gari hilo wakati wa kutokea kwa kisa hicho.
Bw Price alisema ana binti mwingine mkubwa, lakini akasema Patrice alikuwa na bidii sana.

Mwezi uliopita mvulana wa umri wa miaka minne alimpiga risasi mamake Jamie Gilt, katika jimbo la Florida katika tukio linalofanana na hilo, lakini Bi Gilt alinusurika kwa kupata majeraha.

0 comments:

Post a Comment