Thursday, 7 April 2016

BIASHARA YA UKAHABA YAPIGWA STOP UFARANSA.!

Bunge la Ufaransa limeidhinisha sheria mpya, inayopinga biashara ngono nchini humo.

Hatua hiyo inadaiwa kwamba huenda ikaathiri maisha ya watu zaidi ya elfu thelathini, ambao wanategemea shughuli za ngono katika kujipatia kipato ambao wengi wao ni raia wa kigeni.
Chini ya sheria hiyo mpya watu watakaokutwa wakilipia huduma hiyo, wataadhibiwa kwa kulipa dola 1700.
Mmoja wa mbunge anayeunga mkono sheria hiyo, ameitetea na kusema kuwa inalengo la kuhamasisha watu kujiondoa katika biashara hiyo.

Hata hivyo kundi dogo la makahaba waliandamana nje ya bunge, wakipinga sheria hiyo kwa madai kuwa wapewe uhuru wa kujilinda wenyewe, na si kukatazwa kufanya biashara hiyo.

Related Posts:

  • Je umeambukizwa Nomophobia..? Soma utafiti Utafiti wa hivi karibuni uliowachunguza wanafunzi 1000 Korea Kusini, umebaini kuwa asilimia 72 ya watoto wanapata simu wakifikia umri wa miaka 11 au 12. Aidha kwa Wanafunzi hao huzitumia simu hizo za kisasa kwa karibu sa… Read More
  • Papa Francis kurahisisha sheria ya talaka……… Papa Francis anatarajia kurahisisha taratibu zinazoruhusu wafuasi wa kanisa katoliki waliooana kutoa talaka na kuolewa tena huku wakibakia kuwa wafuasi wa katika kanisa hilo. Maelezo ya taratibu hizo yanatarajiwa kutanga… Read More
  • Usikose nakala yako ya gazeti la TABIBU kesho alhamisi kwa bei ya sh. 500/= tu. … Read More
  • Vifo vinavyotokana na nyoka kuongezeka….? Shirika la kimataifa la misaada Medecins Sans Frontieres,limeonya kwamba vifo vitokanavyo na kuumwa na nyoka huenda vikaongezeka. Hali hii inasababishwa na kuisha kwa akiba za dawa inayotibu sumu ya nyoka. Inadhaniwa kw… Read More
  • Utafiti kuchunguza jinsi mtu anavyozeeka…… Vipimo mbalimbali pia huchukuliwa Wanasayansi mjini London wamegundua utafiti mpya,wa kuchunguza utaratibu wa jinsi  mtu anavyo zeeka. Unaangalia tabia ya zaidi mamia ya vinasaba vya damu, ubongo na seli za misuli.… Read More

0 comments:

Post a Comment