Umoja wa Falme za Kiarabu
(Imarati) umeanza kujenga kituo chake cha kwanza cha kijeshi nje ya nchi huko
Eritrea.
Taarifa zinasema kuwa picha za
satalaiti zilizopatikana, zinaashiria kuwepo kituo kimoja kipya cha kijeshi na
vile vile kuendelea ujenzi wa bandari katika uwanja wa ndege wa Assab huko
Eritrea.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo
inaonekana kuwa Imarati hivi sasa inajenga bandari hiyo mpya, pembeni ya uwanja
wa ndege wa kimataifa wa Assab huko Eritrea, ambayo inaweza kuwa kituo cha
kudumu cha kijeshi cha nchi hiyo nje ya Imarati.
Picha hizo za satalaiti zinaonyesha
kwenda kasi kwa ujenzi huo,ulioanza baada ya mwezi Septemba mwaka jana.
Eritrea ni nchi inayopatikana
katika pwani ya bahari Nyekundu kaskazini mashariki mwa Afrika, huku lango la
kistratejia la Babul Mandab likiwa njia ya mawasiliano ya baharini kati ya nchi
hiyo na Yemen.
0 comments:
Post a Comment