Monday 18 April 2016

MWANAMUZIKI AFUTA TAMASHA BAADA YA MBWA WAKE KUUGUA…

Mwanamuziki mmoja kutoka Uingereza, ameahirisha tamasha lake la muziki visiwa vya Caribbean baada ya mbwa wake kuugua.

Joss Stones alisema mbwa huyo kwa jina Missy ni kama mtoto kwake.
Aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kwamba aliahirisha tamasha la Jumamosi Katika kisiwa cha Barbados na Jumanne kisiwa cha Trinidad, baada ya mbwa wake kuanza kuvuja damu.
Amesema anajua uamuzi wake huo unaonekana kama jambo la kushangaza, lakini kwake mbwa huyo ni kila kitu.
Amesema anatumai kufanya onesho nchini Venezuela tarehe 21 Aprili, kama mambo yakiwa sawa.

Stone tayari ameandaa maonesho India, Nepal, Panama na Costa Rica kama sehemu ya safari yake nchi mbalimbali duniani, kuitangaza albamu yake ya saba kwa jina Water For The Soul.

0 comments:

Post a Comment