Thursday 7 April 2016

LEO NI KUMBUKUMBU YA KIFO CHA AMANI ABEID KARUME…

Leo April 7, 2016 ni siku ya kumbukumbu ya miaka 44 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar
Hayati Sheikh Abeid Amani Karume ambaye alizaliwa mwaka 1905 na kufariki tarehe 7 Aprili 1972 kwa kupigwa risasi.
Mzee Karume aliongoza nchi baada ya mapinduzi yaliyomwangusha Sultani, aliyekuwa akitawala Zanzibar hadi mwanzoni mwa mwaka 1964.
Baada ya miezi mitatu Zanzibar iliungana na Tanganyika iliyokuwa ikiongozwa na Mwalimu Nyerere.
Baada ya Muungano wa nchi hizi mbili uliozaa Tanzania, Mzee Karume alikuwa Makamu wa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 
Hayati Sheikh Abeid Amani Karume aliuwawa kwa kupigwa risasi ndani ya ofisi za Makao Makuu ya CCM Kisiwandui, Unguja, wakati akicheza bao na marafiki zake.
Sehemu hii imewekwa uzio maalumu ili kupahifadhi kama kumbukumbu, kwani kila kitu kipo vile vile kilivyokuwa siku hiyo tukio hilo la kuuwawa kwake lilipotokea.

0 comments:

Post a Comment