Tuesday, 26 April 2016

MAELFU WAANDAMANA NORTH CAROLINA….

Maelfu ya waandamanaji wamesafirishwa kwa mabasi hadi katika mji mkuu wa jimbo la North Carolina nchini Marekani ili kufanya maandamano.

Waandamanaji hao wameenda ili kuunga mkono na wengine kupinga sheria mpya ya kitaifa, ambayo inawapa masharti makali watu wa mapenzi ya jinsia moja (mashoga).
Sheria hiyo inasema kuwa watu wanatakiwa kutumia vyoo vya umma, ambavyo vinashabiana na hali yao ya kijinsia ya kuzaliwa sawa na inavyoorodheshwa katika cheti cha kuzaliwa, badala ya namna wanavyojitambua kijinsia.

Sheria hiyo inawalengo wanaume mashoga wanaojisaidia katika vyoo vya umma vya kike, kwa kile wanachosema kuwa wanajitambua kijinsia wao ni wa kike.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment